michezo

Taarifa Za Kifo Cha Mwanasoka Luyanda Ntshangase Aliyepigwa Na Radi.

on

Mwanasoka nchini Afrika Kusini ambaye alipigwa na radi wakati wa mechi amefia hospitalini, klabu yake imethibitisha.

Mshambuliaji huyo wa timu ya Maritzburg United Luyanda Ntshangase, aliyekuwa na umri wa miaka 21, alikuwa katika hali mahututi tangu alipojeruhiwa katika mchezo wa kirafiki tarehe 1 Machi.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa facebook wa klabu hiyo, imemuelezea mchezaji huyo kama miongoni mwa nyota mchanga aliyekuwa aking’ara na kuja kwa kasi kwenye ulimwengu wa soka la nchi hiyo na kwamba klabu hiyo iko kwenye majonzi mazito kufuatia kifo chake.

“Sisi tuna huzuni sana kuhusu kumpoteza Luyanda, mchezaji mchanga mzuri na mwenye uwezo mkubwa,” alisema mwenyekiti wa Maritzburg Farook Kadodia katika taarifa hiyo.

“Kwa niaba ya klabu ya Soka ya Maritzburg United, tunataka kuonesha na kuwapa faraja zetu kwa familia ya Ntshangase.”

 

vyombo vya habari nchini Afrika kusini vinaarifu kuwa mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliopigwa na mwali wa radi wakati wa mechi mjini KwaZulu-Natal, majeruhi wawili waliumia kidogo ingawa Ntshangase aliungua vibaya upande wa kifuani .

Vifo vya wachezaji huyo kwa ajali ya radi hii si mara ya kwanza kwani hii ni mara ya tatu kuikumba timu hiyo ya Maritzburg United katika miaka ya hivi karibuni.

Miongoni mwa waliopoteza uhai kwa njia ya ajali tofauti ni Mondli Cele,aliyekuwa na miaka 27, na Mlondi Dlamini, 20, wote wawili walikufa kwa ajali za gari tofauti mmoja mwaka 2016 na mwingine 2017.

BBC.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *