michezo

Tatoo Ya Sterling Yakosolewa.

on

Mchezaji soka wa England Raheem Sterling ametetea tattoo yake mpya ya bunduki kwenye mguu wake akisema ”ina maana kubwa sana” akimaanisha ina uhusiano na mahrehemu baba yake .

Wanaharakati wanaopinga silaha wamemkosoa mshambuliaji huyo wa Manchester City baada ya kuushirikisha umma picha yake ya tattoo ya silaha hiyo aina ya M16 kwenye mguu wake.

Picha hiyo imetajwa kama “isiyokubalika kabisa” na “inayoudhi”.

Lakini Sterling amesema ni ishara ya kiapo alichoapa kwamba “hatawahi kushika bunduki” baada ya baba yake kupigwa risasi alipokuwa mvulana mdogo.

Sterling, mwenye umri wa miaka 23, ambaye atakwenda Urusi msimu huu kam sehemu ya kikosi cha England kitakachoshiriki Kombe la Dunia , alifichua tattoo yake kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa anafanya mazoezi na wenzake katika St George’s Park.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *