habari

Tayari Angela Merkel Ameapishwa

on

Hapo jana katika bunge la Ujerumani mjini Berlin, Angela Merkel ameapishwa kuwa Kansela wa Ujerumani hatua inayompa mwanya wa kuongoza kwa muhula wa nne.

Merkel alichaguliwa na bunge la Ujerumani -Bundestag, kwa kura 364 dhidi ya kura 315 za hapana. Merkel alihitaji kushinda kura zisizopungua 355 katika bunge hilo lenye viti 709. Vyama vya kihafidhina vya Kansela Merkel vilishinda uchaguzi Septemba mwaka jana kwa asilimia 33 ya kura vikifuatiwa na chama cha SPD kilichopata asilimia 20.5. Merkel mwenye umri wa miaka 63 sasa anaanza muhula wake wa nne kama Kansela wa Ujerumani na muhula wa tatu kama kiongozi wa serikali ya Muungano na kuhitimisha siku 171 za kusubiri serikali mpya ya muungano baada ya uchaguzi wa mwezi  Septemba.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *