michezo

Thomas Tuchel Kocha Mpya Paris Saint-Germain Msimu Mpya.

on

Thomas Tuchel, kocha wa zamani wa timu ya soka ya Ujerumani Borussia Dortmund atakuwa kocha mpya wa timu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain.

Ni kazi ya kwanza nje ya Ujerumani kwa Tuchel mwenye umri wa miaka 44, ambae alipata mafanikio mazuri kwa misimu kadhaa akiwa timu ya Mainz kabla ya kumpokea Jürgen Klopp kama kocha wa Dortmund. Tuchel alilazimika kuacha kucheza soka mnamo mwaka 1998 baada ya kupata jeraha la mguu wakati akiichezea timu ya Ulm.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *