habari

Trump Na Rais Moon Jae-in Wakutana White House.

on

Rais Donald Trump amekutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kwenye ikulu ya Marekani kujadili uwezekano wa kuziondoa silaha za nyuklia za Korea Kaskazini. Viongozi hao wamekutana wakati ambapo pana wasiwasi huenda mkutano kati ya rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wa mwezi ujao ukavunjika.

Hata hivyo Trump amesema anaamini kuwa Kim Jong Un ana dhamira ya kweli juu ya kuziondoa silaha za nyuklia nchini mwake lakini rais huyo wa Marekani alikwepa kujibu maswali kuhusu mkutano wake na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini unaopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi ujao. Wakati huo huo, rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema hatma na mustakabali wa Rasi ya Korea unategemea mazungumzo baina ya Trump na Kim Jong Un.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *