habari

“Tuendelee Kuijenga Amani Yetu, Upendo Wetu Na Tujenge Maendeleo Ya Watanzania Wote” JPM.

on

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania wote kuendelea kuishi kwa amani na upendo huku wakishiriki ipasavyo katika ujenzi wa Taifa.
Rais amesema hayo leo Jumapili baada ya kuungana na Wakristo wote nchini katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
“Kifo na ufufuo wa Bwana Yesu Kristo ukafufue matendo yetu, tuendelee kuijenga amani yetu upendo wetu na tujenge maendeleo ya Watanzania wote, kwani Kristo amefundisha upendo miongoni mwetu.’’
Kwa hiyo nakushukuru sana kwa kuongoza Misa hii naomba ufikishe shukrani zangu kwa kardinali Pengo, maaskofu wote na Watanzania wote tuendelee kusimama pamoja ili kulijenga Taifa letu.’’ amesema Magufuli.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *