habari

“Tufanye Kazi Kwa Ubora Na Wakati” Mhandisi Kamwelwe (MB),

on

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe (Mb) akiongea
na watendaji wa wizara, pamoja na taasisi zake (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika ofisini kwake Dodoma. Waziri Kamwelwe katika kikao hicho amesisitiza kufanya kazi kwa ubora, ndani ya muda mfupi na kutoa huduma kwa wananchi ndio jambo la msingi.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea
na watendaji wa wizara na taasisi zake. Mhe. Jumaa amesisitiza kazi ifanyike kwa pamoja na kufikia lengo la kumtua mama ndoo ya maji nchini.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akitoa neno la utangulizi katika kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa wizara na taasisi zake leo. Prof. Mkumbo amesisitiza utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayowalenga wananchi wa Tanzania ni picha inayojieleza kuwa serikali ipo na wananchi ndio namba moja katika huduma hizo.

Sehemu ya watendaji waliohuduhuria kikao hicho wakimsikiliza Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isac Kamwelwe (Mb), hayupo pichani.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *