habari

Tume Ya Uchaguzi Yaujibu Ubalozi wa Marekani Sakata la Uchaguzi wa Marudio Kuwa na Dosari

on

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekanusha taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani kwamba katika uchaguzi mdogo uliofanyika Agosti 12, mwaka huu uligubikwa na vurugu na uvunjifu wa sheria.

Aidha, Tume pia imeutaka Ubalozi huo kuthibitisha wanachokieleza juu ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kata 36.

Kwa mujibu wa taarifa ya NEC iliyotolewa na Ofisa Habari Mwandamizi wa tume hiyo, Christina Njovu, imesema Ubalozi huo umetoa taarifa inayotoa tuhuma dhidi ya Serikali, tume na Jeshi la Polisi kuwa sheria haikufuatwa na pia ulikuwa na vurugu katika uchaguzi huo.

“Uchaguzi mdogo huwa hauna waangalizi wa Kimataifa, je Ubalozi huo umetoa wapi taarifa hizo? Na hayo waliyoyaona, wameyaona kwa kutumia utaratibu upi na sheria ipi?

“Katika Jimbo la Buyungu mgombea wa Ubunge mmoja wapo kupitia Chadema alijitokeza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na kueleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo, na ameshukuru kwa kuwa Uchaguzi huo umemjenga.

“Kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura, kwa kuwa vurugu hizo zilipelekea jinai kufanyika mbo husika vinashughulikia.

“Aidha, tume inapenda kuufahamisha umma kuwa Tanzania ni nchi huru na inaendesha chaguzi zake kwa mujibu wa Katiba yake na Sheria za Uchaguzi. Kama kuna ambaye hajaridhika bado sheria za nchi zinampa fursa ya kuwasilisha malalamiko yake kwenye mamlaka mbalimbali zilizopo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *