michezo

Uchunguzi Waanza Juu Ya Tuhuma Za Rushwa Dhidi Ya Kocha Msaidizi Wa Nigeria.

on

Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limeanza uchunguzi juu ya madai ya rushwa dhidi ya kocha Salisu Yusuf ambaaye aliiongoza timu ya taifa ya Nigeria kama kocha msaidizi katika mashindano ya kombe la dunia nchini Urusi.

Yusuf (56) alinaswa na kamera akichukua fedha kutoka kwa watu wanaoelezwa kuwa wakala wa mchezo wa mpira wa miguu ambao walikuwa wanataka wachezaji wawili wachaguliwe kwa ajili ya michuano ya mabara.
”Ni kweli kuwa NFF wameanza uchunguzi wa awali kuhusu jambo hilo kusaidi akamati ya maadili”, alieleza mkurugenzi wa mawasiliano Ademola Olajire alipozungumza na shirika la habari la BBC.

Yusuf amejitetea kuwa pesa alizopokea ni zawadi na kuwa wachezaji walichaguliwa kwa kuzingatia uwezo wao.

”Katika madai hayo hakuna sehemu inayoonyesha kuwa niliomba fedha kutoka kwa mawakala,isipokuwa wakala alinipatia pesa baada ya kueleza ‘matumaini’ kuwa wachezaji hao watashiriki michuano hiyo”, Alieleza Yusuf
”Nilipokea fedha hizo kutoka kwa mmoja wa mawakala,ambapo baadae nilibaini kuwa ni dola 750 na si 1000”.

Umoja wa makocha nchini Nigeria wamesema wako upande wa Yusuf ambaye aliiongoza Nigeria katika michuano ya mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Morocco mwaka huu.
Kwa hivi sasa Yusuf anapata matibabu nchini England. Kocha mkuu huyo wa Super Eagles anatarajiwa kuongoza kikosi cha Nigeria kwenye michuano ya Olimpiki mwaka 2020

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *