habari

Ufaransa: Maelfu Waandamana Kupinga Maamuzi Ya Rais Macron.

on

Maelfu ya watu wameandamana jijini Paris nchini Ufaransa kupinga mabadiliko yanayofanywa na serikali ya rais Emmnuel Macron. Maandamano haya yamekuja wakati rais Macron mwenye miaka 40, akidhimisha mwaka mmoja madarakani tangu kuchaguliwa kuwa rais wa taifa hilo la bara Ulaya.

Polisi wa kupambana na ghasia wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2,000 walionekana jijini Paris, huku maandamano mengine yafanyika katika miji ya Kusini ya Toulouse na Bordeaux.Serikali imesema ililazimika kutuma maelfu ya polisi barabarani kwa hofu ya kutokea kwa machafuko na uharibifu wa mali kama ilivyoshuhudiwa wakati wa sikukuu ya wafanyikazi tarehe 1 mwezi huu.

Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa  ongezeko la maandamano nchini Ufaransa kupinga sera mpya za rais Macron kwa watumishi wa umma ikiwemo sekta ya elimu na usafiri hasa wanaofanya katika Shirika la reli.

Rais Macron ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea na mabadiliko hayo, kwa lengo la kuimarisha uchumi wa taifa hilo, licha ya pingamizi kutoka kwa wafanyikazi wa umma.

RFI.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *