habari

Ufaransa: Polisi 9 Wajeruhiwa Katika Maandamano.

on

Maafisa tisa wa polisi nchini Ufaransa wamejeruhiwa wakati wa machafuko yaliyozuka wakati wa maandamano ya kutaka mabadiliko katika sheria za wafanyakazi katika miji miwili nchini humo. Katika mji wa kusini wa Montpellier kituo cha redio cha Franceinfo kimeripoti kwamba kundi la waandamanaji wa mrengo wa kushoto walipambana na maafisa wa polisi kufuatia maandamano ya kuipinga serikali ambapo Wizara ya Usalama wa ndani ya Ufaransa inasema watu 51 walitiwa nguvuni.

Magharibi mwa nchi hiyo polisi 2,500 waliitwa ili kuwaondoa watu katika jengo moja kaskazini magharibi mwa mji wa Nantes ambalo lilikuwa makaazi ya watu kwa miaka kwani jengo hilo ndilo lililotumiwa kwa maandamano ya awali yaliyokuwa yakiupinga mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege.

Kilio cha kubadilishwa kwa sheria hizo za kazi kimewafanya wafanyakazi katika sekta kadhaa ikiwemo wale wa shirika la ndege la nchini Ufaransa Air France pamoja na wafanyakazi wa huduma za reli kuandamana na kusababisha matatizo makubwa kwa wasafiri kote nchini humo.

Na DW.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *