michezo

Ujerumani: Kocha Joachim Atangaza Kikosi Cha Awali Cha Kombe La Dunia

on

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani Joachim Löw, ametangaza kikosi chake cha awali kitakachoshiriki katika mashindano ya kandanda Kombe la Dunia yatakayoanza mwezi ujao nchini Urusi. Shirikisho la kandanda la Ujerumani limeurefusha mkataba wa kocha huyo hadi mwaka 2022.

Kikosi hicho cha wachezaji 27 kitaelekea kambini nchini Australia wiki ijayo ambako kitapiga kambi ya mazoezi kabla ya kuelekea Urusi. Joachim atahitaji kuwatema wachezaji wengine wanne. Mbali na mchezaji wa kiungo wa Borussia Dortmund Mario Götze aliyeachwa nje, hakuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi hicho. Miongoni mwa waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni mlinda lango Manuel Neuer, na Mesut Özil

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *