habari

Ujumbe Wa Papa Francis Kwa Mataifa Ya Syria, Korea Na Gaza.

on

Maelfu ya waumini wa Kikristo ulimwenguni kote wameadhimisha siku kuu ya Pasaka.ambayo ni kumbukumbu muhimu zaidi ya kifo na kufufuka kwa Yesu.

Akiongoza kumbukumbu hizo mjini Rome katika eneo la uwanja wa kanisa la Mtakatifu Petro, mbele ya mamia kwa maelfu ya mahujaji, kiongozi wa kanisa la Katoliki ulimwenguni Papa Francis ametaka maangamizi yanayofanyika Syria yasitishwe haraka na kuwe na maridhiano Mashariki ya Kati.

Papa Francis pia ametoa wito wa maridhiano kati ya Waisrael na Wapalestina, baada ya machafuko yaliyotokea katika ukanda wa Gaza kati ya vikosi vya usalama vya Israel na waandamanaji wa Palestina na kusababisha vifo vya Wapalestina 16 Ijumaa iliyopita.

Pia amezungumzia Kuhusu rasi ya Korea, ambapo amesema anatumai mazungumzo yanayolenga kutuliza taharuki ya muda mrefu yataleta amani katika eneo hilo. Amewahimiza wale wanaohusika moja kwa moja kutumia hekima kwa manufaa ya watu wa Korea na kujenga uhusiano wa uaminifu na jamii ya kimataifa. Ujumbe wa Papa umelenga pia baadhi ya maeneo ya Afrika yanayokumbwa na njaa, machafuko na ugaidi.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *