habari

UNICEF: Zaidi Ya Watoto 1,ooo Wametekwa Na Makundi Ya Kigaidi.

on

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limesema zaidi ya watoto 1,000 wametekwa nyara na makundi ya itikadi kali katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013. Taarifa hiyo ya UNICEF inakuja mnamo wakati Nigeria ikijiandaa na kumbukumbu ya miaka minne tangu tukio la kutekwa nyara wasichana wa Chibok.

Katika taarifa yake UNICEF imesema tangu mwaka 2013 zaidi ya watoto 1,000 wametekwa nyara na kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria wakiwemo wasichana 276 waliochukuliwa kutoka shule ya sekondari katika mji wa Chibok mwaka 2014. Kwa mujibu wa UNICEF kiasi ya walimu 2,295 wameuawa na zaidi ya shule 1,400 kuharibiwa na makundi ya itikadi kali katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *