siasa

Upinzani DRC Wakumbwa Na Malumbano Ya Ndani.

on

Chama kongwe cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo cha UDPS kinaendelea kukumbwa na malumbano ya ndani huku matokeo ya uchaguzi wa Felix Tshisekedi kukiongoza chama hicho, yakiwa yanaendelea kupingwa.

Kupingwa kwa chama hicho kunaratibiwa na Kundi linaloongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala, anayewakilishwa na Tharcisse Loseke, amapo kundi hilo linaendelea kuwa na kutumaini kuwa matokeo ya mkutano mkuu wa chama cha UDPS yatafutwa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Wiki hii Mahakama ya mwanzo ya eneo la Matete itaamua kuhusu ombi lililowasilishwa na kambi ya Tshibala ambayo ilipinga uamuzi uliosainiwa na katibu mkuu wachama cha UDPS wa kuitisha mkutano mkuu wa chama hicho.

Kiongozi wa kundi linaloongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala Tharcisse Loseke, anaamini kuwa mahakama itafuta matokeo ya uchaguzi ambayo yalimuidhinisha Felix Tshisekedi kuongoza chama cha UDPS katika kinyang’anyiro cha urais.

Kwa upande wa wafuasi wa chama cha UDPS inayoongozwa na Felix Tshisekedi, wanasema hawaoni umuhimu wa mahakama kuweza kuipa sheria kambi ya Loseke-Tshibala.

Wakati huo huo, Kambi nyingine ya tatu inayoongozwa na Valentin Mubake, imesema haitambui ushindi wa Felix Tshisekedi katika matokeo ya mkutano mkuu yaliyotangazwa Siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita, huku tume ya kitaifa inayofuatilia makubaliano (CNSA) iliamua na kutaja kuwa uamuzi wa UDPS inayoongozwa na katibu mkuu Jean-Marc Kabund ulikua sahihi.

CNSA iliitaka kambi ya Tshibala-Loseke kuunda chama kipya na kuchagua chenyewe jina tofauti na UDPS, agizo ambalo lilitolewa pia kwa kwa Valentin Mubake na Corneille Mulumba.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *