siasa

Upinzani Nchini Togo Wasitisha Kufanya Maandamano.

on

Upinzani unaoendelea na maandamano Nchini Togo ya kupinga utawala wa rais Faure Gnassingbe kwa miezi saba sasa umetangaza kwamba umefuta maandamano yaliyokua yamepangwa wiki hii nchini humo.

Maandamano hayo yalipangwa kuanza Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lome na katika miji mingne mikubwa. Maandamano hayo hayatofanyika kwa muda wa siku mbili, kwa mujibu wa chanzo kutoka upinzani.

Serikali haikupiga marufuku maandamano hayo, lakini ilikua ilitoa barabara ambazo zingelitumiwa kwa maandamano hayo, hatua ambayo upinzani ulifutilia mbali.

Katika taarifa yake Upinzani nchini Togo, umesema Muungano wa (vyama 14 vya upinzani) umeamua kusitisha kuandamana kwa siku mbili mfululizo kwa ombi la raia wa Togo.

Hata hivyo, upinzani umetoa wito kwa wananchi wa Togo, nchini na wale waishio katika nchi za kigeni, kuwa makini na kuwa tayari kufuata maelekezo ya siku chache zijazo.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *