habari

Urusi Kuomboleza Vifo Vya Watu 64 Kwenye Ajali Ya Moto. Uchunguzi Zaidi Waagizwa.

on

Siku mbili baada ya tukio la moto lililotokea kwenye mji wa Siberian na kusababisha vifo vya watu 64 wakiwemo watoto 41 baada ya kujikuta wamenaswa kwenye jengo hilo, umeibuka ukosolewaji mkubwa kupitia kwenye mitandao ya kijamii. Wakati huo huo utawala wa Kremlin umetangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa siku ya Jumatano huku maswali yakiibuka kuhusu hatua zilizochukuliwa na rais Putin katika kushughulikia janga hilo alilodai kuwa lilisababishwa na uzembe.

Uchunguzi umeagizwa kufanyika na watu watano wanashikiliwa mpaka sasa kuhusiana na moto huo uliounguza karibu nusu ya jengo hilo lililokuwa na maduka makubwa na kumbi za Sinema.

Moto huo ulizuka kwenye maduka yaliyoko kwenye mji wa Kemerovo magharibi mwa Siberian siku ya Jumapili mchana.

Wachunguzi wanasema raia pamoja na wanyama waliungua wakiwa hai au kwa kukosa hewa kwa sababu milango ya dharula ilikuwa imefungwa, ukitolewa mfano ule wa ukumbi wa Sinema ambako watoto ndio walikuwa wengi zaidi.

Rais Putin ametembelea eneo la tukio na kuwaambia maofisa wake amechukizwa na namna kulivyokuwa na uzembe katika kukabiliana na moto huo.

“Nini kinatokea hapa? Hakuna tukio la kijeshi. Hili sio kuwa ni tukio la kuvuja kwa gesi. Watu, watoto walikuja kupumzika,” alisema rais Putin baada ya kuweka shada la maua.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *