habari

Urusi Nayo Yapanga Kulipa Kisasi Kwa Uingereza.

on

Serikali ya Urusi imesema italazimika kuwafukuza wanadiplomasia wa Uingereza ili kulipiza kisasi baada ya Waziri Mkuu Theresa May kuwafukuza wanadiplomasia wake 23 siku ya Jumatano.

Waziri wa Mambo ya nje Sergei Lavrov amesema inasikitishwa na uamuzi wa Uingereza kuilaumu Urusi kwa kumpa simu aliyekuwa jasusi wake Sergei Skripal pamoja na binti yake Yulia. Lavrov amesisitiza kuwa Urusi itachukua hatua hiyo na kuongeza kuwa anayeweza kuwafukuza wanadiplomasia wa Uingereza ni rais Vladimir Putin. Uingereza ilichukua hatua ya kuwafukuza wanadiplomasia wake baada ya Urusi kushindwa kueleza ni kwanini walimpa sumu Skripal baada ya uchunguzi kuonesha hilo.

Jasusi huyo wa binti yake wanaendelea kupata matibabu na hali yao ni mbaya. Marekani imesema inaunga mkono hatua ya Uingereza ambaye ni mshirika wake wa karibu na kusema kuwa inaamini kuwa Urusi ndio iliyohusika.

Naye rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema serikali yake itatangaza hatua za kuchukua katika siku zijazo dhidi ya serikali ya Moscow. Rais Macron amesema kitendo cha Urusi hakikubaliki na kinastahili kulaaniniwa.

“Nitatangaza hatua za kuchukua katika siku zijazo,” alisema rais Macron. Kiongozi huyo wa Ufaransa atajadili suala hili na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye atazuru jijini Paris siku ya Ijumaa.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *