habari

Venezuela: Wafungwa 68 Wapoteza Maisha Wakijaribu Kotoroka.

on

Watu 68 wamekufa nchini Venezuela wakati walipojaribu kutoroka kwenye jela moja baada ya moto kuzuka kwenye vyumba ambavyo walikuwa wakizuiliwa na Polisi, hili likiwa tukio baya zaidi kuripotiwa kwenye jela lenye ulinzi mkali na lenye idadi kubwa ya wafungwa.

Mwanasheria mkuu wa Serikali Tarel William ametoa idadi hii usiku wa kuamkia leo kwenye makao makuu ya polisi kaskazini mwa mji wa Carabobo, akilaumu kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi.

Carlos Nieto mkuu wa gereza hilo amesema baadhi ya wafungwa waliungua hadi kufa na wengine kwa kukosa hewa baada ya moto kuanza kuunguza magodoro na kuanza kuiba slaha kutoka kwa walinzi wakijaribu kutoroka.

Miongoni mwa waliokufa ni wanawake wawili ambao walienda kuwatembelea ndugu zao, amesema mwanasheria mkuu ambaye amedai kuwa waendesha mashtaka wanne wameteuliwa kuchunguza tukio hili.

Picha zilizopigwa na vuguvugu la Nieto limeonesha askari wa zima moto wakijaribu kumuokoa mfungwa mmoja aliyekuwa akiungua.

Ndugu wa watu waliokuwa wanazuiliwa kwenye kituo kimoja walilazimisha kuingia baada ya polisi mmoja kupigwa jiwe ambapo baadae polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Video iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa twitter umeonesha mamia ya watu wakiomba kupewa taarifa kutoka kwa polisi waliokuwa wanalinda jela hiyo huku wanawake wakilia.

“Nina hofu. Mwanangu amekuwa hapa kwa karibu wiki moja. Hawajanipa taarifa zozote,: alisema Dora Blanco.

Wafungwa wengi nchini Venezuela wanataabika kutokana na hali mbaya za magereza, kukosekana kwa mahitaji muhimu ya kibinadamu na jela kujaa kupita kiwango huku wakikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *