siasa

Vijana Wa Chama Tawala Burundi Waandamana.

on

Vijana zaidi ya elfu mbili kutoka chama tawala nchini Burundi maarufu kama Imbonerakure wamefanya maandamano katika jimbo la Muyinga kaskazini mashariki mwa nchi hiyo usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi.

Wakazi wa maeneo ya karibu na yalipofanyika maandamano hayo, kwa masharti ya kutotajwa majina yao, wameliambia shirika la habari la Afp Kwamba walishtushwa na sauti za nyimbo miluzi na michezo kadhaa ya vijana wa Imbonerakure waliokusanyika kuanzia saa nane za usiku.
Vijana wa rika mbalimbali waliendelea kukusanyika hadi saa kumi na mbili asubuhi kabla ya kujikusanya katika uwanja wa mpira wa miguu na kutoleana hotuba mbalimbali.

Kundi la vijana wa chama cha CNDD FDD Imbonerakure wamekuwa wakitajwa kuingilia usalama wa nchi hiyo kwa kudhibiti na kuzuia uvukaji wa mipaka kuingia nchi jirani za Rwanda na Tanzania hasa kwa warundi wanaojaribu kutafuta hifadhi huko.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *