siasa

Viongozi Wa Chadema Wamewasili Kituo Kikuu Cha Polisi. (Centro).

on

Viongozi wa Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho Vincent Mashinji, wameripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi (Centro) kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa kwenye kesi yao uchochezi inayowakabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mara baada ya kutoka ndani ya kituo hicho, mbele ya wanahabari Mashinji amesema kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya pindi wanaporipoti kituoni hapo, ni kuitikia wito na kusaini kwenye kitabu kilichopo kwenye kituo hicho na baadaye kuondoka kila Ijumaa. Wabunge wengine waliowasili ni Peter Msigwa, John Heche na Ester Matiko.

Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na manaibu wake wa Bara na Zanzi­bar, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wote wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo mawili ya uchochezi wa uasi yanayom­kabili Mbowe.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *