habari

“Viongozi Wa Dini Wasiwe Na Taharuki Na Taarifa Hizo, Hazina Baraka Za Serikali”-Mwigulu.

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema barua iliyoandikwa na wizara hiyo ya kulitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) kuufuta waraka wa Pasaka ni batili.

Dkt Nchemba amesema hayo leo Juni 8 katika mkutano na wanahabari, na kusema kwamba taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa na mkanganyiko wa anuani, na ni batili na siyo maelekezo ya serikali au wizara.

“Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali. Wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake.” Amesema.

Aidha amewaomba viongozi wa dini nchini waendelee na kazi zao, na kwamba jamii inatakiwa iwe macho katika kuchuja taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, na wasifanyie kazi taarifa hizo bila kuwa zimethibitishwa.

Katika hatua nyingine Dr. Nchemba amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, ili kupisha 2018 ili kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT).

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *