habari

Vyama Vitatu Vya Upinzani Vyaridhia Kushiriki Uchaguzi Mkuu.

on

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vyama vitatu vya upinzani vimetangaza kuwa vitashiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwishoni mwa mwaka huu bila ya kumtaja kiongozi aliye uhamishoni Moise Katumbi ambaye wiki hii alitangaza nia yake ya kuwania urais.

Vyama vya UDPS kinachoongozwa na Felix Tshisekedi na MLC cha Jean-Pierre Bemba na kile cha spika wa zamani Vital Kamerhe UNC vimethibitisha nia yao ya kushiriki uchaguzu wa Desemba 23 mwaka huu katika taarifa yao ya pamoja.

Viongozi hawa pia wameeleza kuguswa na hali duni ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo pamoja na kutokuwa na imani na mitambo ya uchaguzi ya Kielektroniki wanayidai kuwa huenda ikawa imeshawekewa taarifa kukisaidia chama tawala.

Katika taarifa yao vyama hivi havikutaja popote jina la Katumbi wala kuonesha kuwa wamejiunga kwenye vuguvugu lake alilolizindua juma lililopita jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Katumbi ambaye ametangaza kuwa atarejea nyumbani hivi karibuni, ili kuanza mchakato wa kuwania urais mwezi Desemba mwaka huu.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *