habari

Waandishi ‘Feki’ Wakamatwa Australia.

on

Zaidi ya watu 50 kutoka Ghana waliokuwa wakijaribu kuingia nchini Australia kwa kudai kuwa ni waandishi wa habari wanaoenda kuripoti habari za mashindano ya madola (Commonwealth games) wameripotiwa kukamatwa baada ya kushindwa kujibu maswali rahisi kuhusu michezo.

Watu hao waliobainika kuwa walijidai kuwa waandishi ili wapate kuingia nchini humo kirahisi walishikiliwa na baadaye kufukuzwa licha ya kuwa na nyaraka zote sahihi za kusafiria.

Taaarifa kutoka kwa maafisa wa polisi zinasema maafisa wa uhamiaji walibaini njama za watu kuingia nchini humo kwa mgongo wa mashindano hayo huku wakiwa na shughuli zao binafsi, hivyo waliandaa maswali ambayo ni ya kawaida kwa watu wanaofuatilia michezo.

Naibu Waziri wa Michezo wa Ghana, Pious Enam Hadidze, amesema kuwa wameanza kufanya uchunguzi kuhusu sakata hilo ili kubaini kama kuna udanganyifu uliofanyika katika kuwapa vibali.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *