habari

Wabunge Urusi Waandaa Mswaada Kupinga Ushirikiano Na Marekani.

on

Wabunge nchini Urusi wamefahamisha leo kwamba wameandaa muswaada wa kujibu vikwazo vipya vya Marekani ambao unapendekeza kupigwa marufuku bidhaa pamoja na huduma zinazotokea nchini Marekani.

Muswaada huo pia unalenga kuweka sheria kali katika ushirikiano wa kiuchumi na nchi hiyo. Muswaada huo unatarajiwa kujadiliwa bungeni wiki ijayo. Bidhaa ambazo zinalengwa katika muswaad huo ni pamoja na Software na bidhaa za kilimo,dawa ambazo zinaweza kupatikana katika maeneo mengine sambamba na Tobacco na mvinyo.

Wabunge wa Urusi pia wamesema kwamba wamependekeza kupiga marufuku ushirikiano na Marekani katika suala la nguvu za atomiki,pamoja na utengenezaji wa mitambo ya roketi na ndege. Kampuni za Kimarekani pia zitazuiwa kushirikiana na Urusi katika mikataba ya kibinafsi kwa mujibu wa muswaada huo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *