michezo

Wachezaji wanne wanaokipiga kimataifa waitwa Taifa Stars

By

on

Kocha wa Timu ya Taifa ya Soka Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga, leo Machi 8, ametaja majina ya wachezaji 23 watakaoingia kambini kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki mwezi huu.

Katika orodha hiyo aliyoitaja asubuhi hii kwenye makao makuu ya shirikisho la soka nchini TFF Karume Ilala, Mayanga amewajumuisha kikosini nyota wanne wa kimataifa akiwemo nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu anayechezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden, Mlinzi wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda na Faridi Mussa anayechezea Club Deportivo Tenerife ya Hispania.

About mjengwa

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *