habari

Wakili Wa Kujitegemea Atajwa Miongoni Mwa Wagombea Urais TLS.

on

Fatma Karume ambaye ni wakili wa kujitegemea, ametajwa kuwa miongoni wa wagombea wa urais Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikiwa inashikiliwa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anayepatiwa matibabu nchini Ubelgiji baada ya kushambuliwa na risasi.

Mbali na Fatma Karume wengine waliotajwa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika April 14, 2018 jijini Arusha, ni Makamu Rais wa TLS, Godwin Ngwilimi, Godwin Mwapongo na Godfrey Wasonga, huku Rugemeleza Nshalla akiwa amepitishwa kuwania umakamu wa urais wa chama hicho cha mawakili Tanganyika.

Kwa upande wake Fatma Karume ameeleza kuwa endapo atashinda na kuwa rais wa TLS, atasimamia haki, utawala bora, na atahakikishia anasimamia vyema misingi ya demokrasia inayowajibika kweli.

Aidha Machi 12, mwaka huu kamati ilikutana na kuyapitia majina yote yaliyopendekezwa na kuwateua wagombea hao kuwania kiti hiko cha urais wa Mawakili Tanganyika.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *