habari

Wananchi Wa Burundi Wapiga Kura Ya Maoni Ya Kurekebisha Katiba.

on

Raia nchini Burundi leo wamepiga kura ya maoni juu ya mabadiliko ya katiba, yatakayompa nafasi Rais Pierre Nkurunziza kuweza kutawala hadi 2034. Hatua hiyo imezua hofu ya ukandamizaji mkubwa wa kisiasa na migogoro ya kikabila katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Wanasiasa wa upinzani na makundi ya kutetea haki za binadamu wametaja mifano mingi ya ukandamizaji, ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa wapinzani, kuzuiwa maandamano ya umma, na vitisho vya vifo kutoka kwa Imbonerakure, tawi la vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD cha Nkurunziza.

Nkurunziza, mwalimu wa zamani wa riadha na aliyekuwa kiongozi wa vita vya msituni kutoka katika kabila la wengi la Hutu, amekuwa akiliongoza taifa hilo tokea mwaka 2005 vilipomalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya watu 300,000.

Pendekezo la kuongeza muda wa kuwa rais kutoka awamu ya miaka tano hadi saba, ambayo itamwezesha Nkurunziza, ambaye amekuwa uongozini tangu mwaka wa 2005, kuendelea usukani kwa miaka mingine kumi na nne muda wake utakapokamilika mnamo mwaka wa 2020.

Serikali hata hivyo imekanusha madai kwamba hilo ndilo lengo kuu, ikisema mabadiliko yanayopendekezwa ni ya kulainisha katiba.

Burundi imebadilisha katiba yake mara kadhaa miaka ya hivi karibuni- Miaka mitatu iliyopita rais Nkurunziza alifanikiwa kujiongezea muda zaidi ya miaka kumi iliyotarajiwa, hali ambayo ilileta maandamano yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 700 huku wengine wapatao 400,000 wakitoroka makwao baada ya msako wa serikali.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *