habari

Watumishi Walioondolewa Kwenye Mfumo Wa Malipo Ya Mshahara, Kurejeshwa Kazini.

on

Waziri wa nchi, ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala bora), George Mkuchika amesema Serikali imewarejesha kazini watumishi walioondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mshahara kwa kukosa sifa ya cheti cha kufaulu mtihani wa elimu ya kidato cha nne.
Kauli hiyo imetolewa na waziri huyo bungeni leo Aprili 9, 2018, ambapo amesema watumishi wote wenye ajira za kudumu au ajira za mikataba (kwa watendaji wa vijiji na mitaa), au ajira za muda waliokuwa kazini kabla ya Mei 20, 2004 ulipoanza kutumika waraka wa utumishi namba moja wa mwaka 2004, warejeshwe kazini mara moja.
Mkuchika amesema Serikali imeagiza watumishi hao walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, Mkuchika amesema Serikali haitawarudisha kazini watumishi waliothibitika kughushi vyeti vya kidato cha nne na kwamba, waliowapa ajira watachukuliwa hatua. Amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Serikali kupokea mapendekezo na malalamiko kutoka vyama vya wafanyakazi na kwa watumishi hao.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *