habari

Waziri Mwalimu Azindua Dawa Mpya ya TB kwa Watoto.

on

Katika kuelekea  siku ya kifua kikuu duniani Tarehe 24 March 2018, Waziri wa Afya Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amezidua dawa mpya ya kifua kikuu kwa watoto pamoja na kukabidhi mashine za kutambua ugonjwa huo kwa vituo vya afya vya binafsi kama hatua ya serikali katika kupambana na ugongwa huo. Maadhimisho hayo ya mwaka huu yana kauli mbiu inayosema VIONGOZI TUWE MSTARI WA MBELE KUONGOZA MAPAMBANO YA KUTOKOMEZA TB.

Awali waziri Ummy Malimu alieleza athari za kifua kikuu hapa nchini. “Kwa kujibu wa taarifa za wizara ya Afya mwaka 2016, takribani watu million 1.3 walifariki dunia kwa ugonjwa wa TB na hapa nchini takwimu tulizonazo zinaonyesha kwamba jumla ya vifo vinavyotokea miongoni wa hao wenye matatizo ya kifua kikuu kwa mwaka ni vifo elfu 28 sawa na vifo 77 kila siku”

Aidha waziri Mwalimu amekabidi mashine 5 zenye thamani ya shilingi Million 35 kila mashine moja, kwa vituo vya afya vitano vya binafs kwa ajili ya kutoa vipimo kwa wagonjwa wa TB.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *