habari

WAZIRI UMMY AKABIDHI MADAWATI 40 SHULE YA SEKONDARI CHUMBAGENI JIJINI TANGA

on

IMG_1045
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akiwa amekaa kwenye mmoja ya madawati 40 aliyoyakabidhi leo kwa shule ya Sekondari Chumbageni kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi ambaye alimuomba Waziri huyo madawati hayoi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo
IMG_1035
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kuwakabidhi madawati hayo
IMG_0996
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
IMG_0835
Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwapa msaada huo
IMG_0917
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuisaidia shule hiyo
IMG_0843
Mwalimu Mkuu wa wa shule ya Sekondari Chumbageni Kavumo Juma Mziray akitoa hotuba yake
IMG_0814
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash wakiimba wimbo wa Taifa
IMG_0752 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akisalimiana na walimu wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kuwasili shuleni hapo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash
IMG_0799 Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakifutiliana makabidhiano hayo
IMG_0857 Sehemu ya madawati na viti ambayo yamekabidhiwa leo na Waziri Ummy kwa shule ya Sekondari Chumbageni
IMG_0858IMG_1102
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kukabidhi madawati hayo leo
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) leo amekabidhia madawati 40 na viti katika shule ya sekondari ya Chumbageni Jijini Tanga ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu zinapatiwa ufumbuzi.
Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika leo shuleni hapo na kuhudhuriwa na walimu, wanafunzi na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ,Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi wakiwemo viongozi wengine. Hatua ya kukabidhiwa madawati hayo shule ya Sekondari ya Chumnageni ilitokana na ombi la Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi ambaye alimueleza waziri Ummy uwepo wa uhaba wa madawati kwenye shule hiyo.
Akizungumza namna alivyoweza kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo, Waziri Ummy alisema baada ya ombi hilo aliwapata wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao walilikubali na kumpatia kiasi cha sh, milioni 5.4 ambazo wameweza kununua madawati 40 na viti “Mh Saida umetenda wajibu wako ipasavyo maana taarifa ya mkuu wa shule inasema kuna uhaba wa viti 163ubawa wa meza 100 hivyo kupatina kwa hivyo vilivyokabidhiwa leo kumepunguza nusu lakini nitaendelea kushirikiana nanyi “Alisema
“Kazi nzuri inafanywa kwenye shule ya sekondari Chumbageni na nimeambiwa kiwango cha ufaulu kinaongezeka mwaka hadi mwaka asilimia 51 hadi asilimia 77 lakini pia nitoe pongeze kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutatua changamoto ya elimu sio watu kusubiri mpaka serikali kuu kwani wamekuwa wakijiongeza na diwani Saida kutatua changamoto ya elimu kwenye kata yake “Alisema.
Hata hivyo alisema ataendelea kushirikiana na madiwani kuhangaika ili aweze kupata fedha za ujenzi wa ofisi ya walimu kwen ye shule hiyo lakini pia wanafunzi nitawaletea vitabu huku akitoa wito kwa wananchi kushirikiana kuona namna ya kutatua changamoto ya elimu sio kusubiri serikali pekee bali ni watu wote.
“Nimshukuru Rais kuanzisha sera ya elimu bure ambayo imewasaidia, watu wengi …watu walikuwa wanaponda shule za kata wakati mimi nilipokuwa nasoma shule zikuwa chache kutokana na kukosekana nafasi lakini leo hii zipo za kutosha hivyo kuwasaidia watoto wa kike kuepushwa na ndoa za utotoni na wavulana kuvuta bangi.
Alisema leo hii Serikali chini ya Rais Dkt John Magufuli imekuwa ilileta milioni 161 kila mwezi kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa ajili ya elimu bure hii imesaidia sana lakini wengine walikuwa wanakosa kwa sababu ya ada lakini tatizo la ada limetatuliwa .
Alisema ndio maana kabla ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani wanafunzi waliokuwa wanaanza kidato cha kwanza Jiji la Tanga walikuwa 4120 lakini leo watoto 6300 kwa sababu ya elimu bure wameweza kupatiwa elimu hivyo hao watoto wangekuwa nyumbani, elimu ndio nyenzo ya kuwaletea maendeleo
Naye kwa upande wake Diwani wa kata ya Chumbageni Saida Gadafi alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada huo wa madawati ambao ulikuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi kwenye shule hiyo na nimuhaidi tutayasimamia vizuri ili yaweze kutumika kwenye malengo yaliyokusudiwa kwa matumizi ya wanafunzi
“Nikushukuru sana Mh Waziri kwa kunisaidia suala hili ambalo ni muhimu sana niwaombe ndugu zangu wanafunzi tumuombee mungu waziri amjalie kilalaheri na mafanikio kwenye shughuli zake za kila siku “Alisema
Awali aklizungumza kwenye halfa hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash alimshukuru sana waziri huku akieleza namna wakazi wa mji huo wanavyohitaji kushirikiana naye kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
“Nikushukuru sana Mh Waziri kwatatulia changamoto ya elimu kwenye shule yetu kwani msaad huu ni mkubwa na ninahaidi kushirikiana nawe katika kila jambo sisi tupo tayari “Alisema

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *