habari

Waziri Wa Mambo Ya Ndani Wa Uingereza Ajiuzulu.

on

Amber Rudd Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza  ametangaza kijiuzulu hapo jana Jumapili kufuatia kashifa dhidi ya maafisa wa nchi hiyo kuwahusisha kimakosa wahamiaji kutoka nchi za Carribean na sehemu ya mchakato wa kuwaondoa wahamiaji wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Waziri Mkuu Theresa May amekubali kujiuzulu kwa Amber Rudd ambaye amekuwa akishinikizwa na chama cha Labor kujiuzulu alikuwa akitarajia kutoa maelezo bungeni leo Jumatatu kuhusiana na kashifa hiyo iliyogonga vichwa vya habari nchini Uingereza kwa siku kadhaa. Kashifa hiyo inafuatia gazeti la Guardian kuripoti kuwa baadhi ya watu waliohamia Uingereza wakitokea nchi za Carribean miongo kadhaa iliyopita baada ya vita kuu vya pili vya dunia wanatishiwa kufukuzwa kutokana na kutowasilisha nyaraka zinazothibitisha kuwa wana haki ya kuendelea kusalia nchini humo.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *