siasa

Waziri Wa Mambo Ya Nje Athibitisha; Raia Waishio Nje Ya DRC Hawatapiga Kura.

on

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kupitia waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo imesema kuwa raia wa DRC waishio ugenini hawatoshirikishwa katika zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mnamo mwezi Desemba mwaka huu nchini humo.

Waziri huyo Emmanuel Ilunga, ameliambia shirika la habari la RFI kwamba muswada wa sheria kuhusiana na hatua hiyo utawasilishwa bungeni ili kupitishwa.

“Ni gharama ya kifedha ya uchaguzi huo na matatizo ya vifaa ambayo inaelezea hatua hiyo, ” amesema Bw Ilunga. “Uchaguzi utafanyika, lakini kwa bahati mbaya, kwa maoni yangu, raia waishio ugenini hawatoshiriki uchaguzi huo … wako nje ya nchi na hakutakuwa na kituo cha kupigia kura nje ya nchi. Wale ambao wanataka kupiga kura wanaweza kuja nchini, kuchukua kadi na kurudi kupiga kura nchini hapa, ” ameongeza waziri wa mambo ya nje wa DRC, na kudai kwamba haiwezekani, hadi mwezi Desemba, tarehe ya uchaguzi, kuandaa uchaguzi katika nchi 180 wanakoishi raia wa DRC.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *