habari

YANGA YAKAMILISHA USAJILI WA KIUNGO MSHAMBULIAJI TOKA MTIBWA SUGAR

on

36963145_268247897258720_5828812319127240704_n

Mabingwa wa Kihistori wa Tanzania klabu ya Yanga imekamilisha saini ya Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar na Mtibwa Sugar,Mohammed Issa Banka kwa mkataba wa miaka miwili wa  kuwatumikia wanajangwani hao.

36887847_2192309804144874_2055627474498224128_n
‘Mo Banka’ ametambulishwa leo Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh aliyeambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani mjini Dar es Salaam.

36963145_268247897258720_5828812319127240704_n

Kuwasili kwa Banka Yanga imepata mchezaji muhimu katika eneo la kiungo Mchezeshaji wa timu na ataungana na kwenye kambi ya mazoezi inayofanyika katika uwanja wa Polisi Kurasini wakijiandaa na michezo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
Yanga inaendelea na mazoezi na kujifua kwa nguvu kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa Juni 18 jijini Nairobi nchini Kenya na ikumbukwe Mechi mbili ambazoimeshuka dimbani hajapata ushindi wa aina yoyote katika michuano hii.
Usajili huo umekamilika ikiwa ni siku kadhaa zimepita baada ya kuwaongezea mikataba wachezaji wake, kipa Beno Kakolanya na beki wa kulia Juma Abdul pamoja na kumrejesha aliyekuwa kiungo wake, Deus Kaseke kutoka Singida united.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *