michezo

Zifahamu Rekodi Za Nadir Harub Cannavaro Kabla Ya Kustaafu Soka

on

Akizaliwa Feburuari 10 ya mwaka 1982, miaka 36 iliyopita katika mitaa ya Michenzani Zanzibar,Cannavaro alikuwa akicheza uwanjani nafasi ya beki wa pembeni kulia lakini pia kama beki wa kati.

Amecheza soka zaidi ya miaka 20 akivitumikia vilabu viwili tu vya hapa hapa nchini Tanzania ambavyo ni Malindi FC kutoka Zanzibar pamoja na klabu ya Yanga ya Dar Es Salaam ambayo kaitumikia kwa muda mrefu zaidi.

Akiwa Malindi Cannavaro alifanikiwa kuitmikia kwa kipindi cha miaka miwili tu kuanzia mwaka 2003-2005 akicheza michezo 36 tu.

Baada ya kucheza Malindi,Yanga waliamua kumrejesha Nadir kuanzia mwaka 2006 ambapo alidumu Yanga mpaka hivi sasa alipoamua kustaafu akifanikiwa kucheza zaidi ya michezo 119 pia akiifungia Yanga zaidi ya agoli 7.

Licha ya kuwa mzaliwa wa Zanzibar Cannavaro alifanikiwa kuitumikia pia timu ya taifa ya Tanzania kuanzia mwaka 2006 akicheza zaidi ya michezo 51 lakini pia wakati huo huo alikuwa akiitumikia timu ya Zanzibar heroes.

Kwa muda wote huo Cannavaro akiwa Yanga alifanikiwa kuwasaidia Wanajangwani hao kutwaa mataji 8 ya ligi kuu kuanzia mwaka 2006,2008,2009,2011,2013,2015,2016,na 2017.

Pia akiisaidia kutwaa taji la ngao ya jamii kwa nyakati nne tofauti kuanzia mwaka 2010,2013,2014,na 2015,Kagame Cup mara mbili mwaka 2011 na 2012 na kombe la Azam Sports Federation mara moja mwaka 2016/17.

Jana Nadir Harub Cannavaro ameagwa rasmi na klabu yake ya Yanga mjini Morogro katika mchezo uliochezwa na vilabu viwili ambavyo ni Yanga pamoja na Mawenzi Market huku Yanga wakifanikiwa kushinda mchezo huo kwa goli la Makambo dakika ya 53.Lakini pia wakitangaza tarehe 19 mwezi huu Cannavaro ataagwa katika uwanja wa taifa Jijini Dar Es Salaam.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *