siasa

Zimbabwe Yazindua Rasmi Kampeni Za Uchaguzi Mkuu.

on

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa jana amekitaka chama chake cha ZANU-PF kuomba kura kwa unyenyekevu wakati ambapo amezindua kampeni yake mbele ya uchaguzi unaotarajiwa mwezi Julai mwaka huu. Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza bila Robert Mugabe kuwa mamlakani tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.

Mnangagwa alichukua mamlaka mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya Mugabe mwenye umri wa miaka 94 kuondolewa madarakani baada ya jeshi kuchukua mamlaka kwa muda mfupi. Chaguzi zilizopita nchini Zimbabwe zimekumbwa na wizi wa kura, vitisho na machafuko ikiwemo kuuwawa kwa wafuasi wa upinzani mwaka 2008.

Mnangagwa ameahidi kufanyika kwa uchaguzi ulio huru na haki wakati ambapo anatafuta kujenga upya uhusiano na jumuiya ya kimataifa ingawa yeye mwenyewe pia amehusishwa na machafuko ya uchaguzi yanayohusishwa na chama cha ZANU-PF.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *