habari

Zitto Kabwe Aipa Ujumbe Mzito CCM Kuhusu Rushwa Kwenye Chaguzi Mbalimbali

on

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amefunguka kuwa suala la rushwa limepigiwa kelele sana na vyama vya upinzani nchini, hivyo basi chama tawala kilitazame hilo kupitia vikao vyake vya ndani.

Zitto amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa ‘twitter’ ambapo ameandika kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally azungumzie mambo yanayoendelea nchini katika vikao vya ndani na asiishie kuzungumza kwenye majukwaa ya nje pekee.
“Upinzani umelalamika sana suala la rushwa kwenye uchaguzi, tuangalie hili suala la chaguzi za marudio. Wananchi wamechoshwa na siasa za hamahama ya wabunge na madiwani, hilo nalo mwalimu Bashiru alizungumzie kwenye vikao vya CCM”, ameandika Zitto.
Ameongeza kuwa , “Siasa za nyimbo za mbele kwa mbele ni za CCM, sasa ni vyema mwalimu Bashiru akaeleza hayo katika vikao vya kamati Kuu na Halmashauri kuu ya chama chake, asiishe kwenye MVIWATA”.
Hayo yamekuja baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally kudai kuwa vitendo vya rushwa na kutowajibika vimesababisha wananchi kupuuza uchaguzi na kuuona kama maigizo hivyo kupelekea idadi ya kura za chama chake kupungua kutokana na wapiga kura kutokuwa na imani na uchaguzi.
Dkt. Bashiru alitoa kauli hiyo Oktoba 4, 2018 mjini Morogoro katika Kongamano la Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) alipokuwa akizungumzia kuhusu umuhimu wa wananchi kuiwajibisha serikali.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *