We have 338 guests and no members online

Matangazo Mapya

We provide the full IT solutions including web design, web development ...

 Mwenge wa Uhuru ukiwasili kwenye uwanja wa mpira wa Mchinga I,wilaya ya Lindi vijijini ambapo ulizindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika Majimbo mawili wa wilaya hiyo, jimbo la Mchinga na jimbo la Mtama.

 Viongozi mbali mbali wakiwa wamesimama tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Lindi Vijijini

 Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Bw. George Jackson kitaifa akizindua mradi wa maji katika shule ya msingi Mchinga I.

 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda wakiwaongoza waongoza Mwenge wa Uhuru kitaifa kupita juu ya daraja lililofunguliwa rasmi na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Daraja hili linawaunganisha wakazi wa Mchinga II na Mchinga I.(P.T)

Read more...

NAPE AMJULIA HALI BABA WA DIWANI WA CHADEMA

Published in Jamii

 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na  Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile (CHADEMA) mara baada ya kuwasili kwenye hospitali ya Nyangao kumjulia hali Baba wa Diwani huyo aliyelazwa hapo. .

 Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipewa maelezo juu maendeleo ya hali ya Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile (CHADEMA) aliyelazwa katika Hospitali ya Nyangao.

Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimuangalia Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile aliyelazwa katika hospitali ya Nyangao.

Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amemjulia hali Mzee Omary Nyimbile, baba wa Diwani wa kata ya Mtama Bw. Hassan Omary Nyimbile .

Mhe. Nape ambaye yupo kwenye ziara ya utekelezaji wa ahadi zake jimboni kwake na kuonana na wananchi alifika kwenye hospitali ya Nyangao mwishoni mwa wiki iliyopita na kupokelewa na Diwani huyo wa kata ya Mtama kupitia Chama Cha Chadema.

Mheshimiwa Mbunge wa Mtama alimjulia hali Mzee Omary na kumtakia heri ya kupona haraka.

Kitendo cha Mhe. Mbunge kumjulia hali baba wa Diwani wa Chadema kimewashangaza wengi ambao walidhani viongozi hawa hawatoweza kuzungumza kutoka na hali ilivyokuwa wakati wa uchaguzi.(P.T)

ke1

Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akitoa neno la ufunguzi katika mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mei 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ke2

Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Christopher Chusi akichangia hoja wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa uliofanyika Mei 30, 2016 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ke3

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wakifuatilia mada ya Menejimenti ya Maafa kutoka kwa Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. John Kiriwai (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ke4

Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Naima Mrisho akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya maafa katika zoezi la ukakamavu katika kujiandaa na kukabili maafa wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa Wilayani Kilosa tarehe 30 Mei, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)

Read more...

UONGOZI Chuo Kikuu cha Dar es salam unatarajia kununua taa za dharura 12 kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la giza katika Hosteli ya Mabibo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anaeshughulikia masuala ya Utawala Prof.David Alfred Mfinanga wakati wa mahojiano na Idara ya Habari.

Alisema kuwa tatizo la giza nene katika eneo hilo la lango kuu la kuingia Hostel za mabibo mpaka eneo lile la maegesho ya magari lipo mbioni kupatiwa ufumbuzi baada ya taratibu za ununuzi kukamilika.

Alisema kuwa kukamilika kwa uwekaji wa taa hizo za dharura zitapunguza kabisa tatizo hilo.

Aidha, Prof.David Alfred Mfinanga alisema kuwa katika mpango wa muda mrefu wa kutatua tatizo hizo uongozi wa UDSM unatarajia kuweka umeme wa jua ambao utapunguza gharama za kulipia umeme na hivyo kuwa na umeme wa uhakika.

Hostel hizo za kisasa zilizojengwa miaka michache iliyopita na Shirika la Hifadhi za Jamii(NSSF) zimesaidia kupunguza tatizo la makazi lililopo kampasi kuu ya Chuo kikuu(mlimani) lakini kasoro hizi za kukosa umeme zinahatarisha eneo hilo kugeuka kuwa la ubakaji na hata ukabaji kwa wanafunzi na wageni.

Imeandaliwa na Daudi Manongi-MAELEZO.  (P.T)

Tafadhali Usinukuu:

Published in Jamii

" Afrika majipu mengine ni ya kujitakia. Kiongozi unapaswa kutafakari kwanza halafu kusema, na si kusema halafu kutafakari.
Kiongozi uwajue kwanza unaowaongoza. Jiulize, unaowaongoza ni watu wa namna gani na wako katika hali gani.

Naam, naziona ishara za maanguko makubwa, tena kwa viongozi wenye nyadhifa kubwa. Ni kama ilivyowatokea wengine, kwa(P.T)

CHU1

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.

CHU2

Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatuma Mrisho akielezea umuhimu wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 katika mkutano wa wadau wa utafiti huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.

CHU3

Mkurugenzi Mkazi wa ICAP Tanzania Dkt. Fernando Morales akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti, 2016.(P.T)

Read more...

MAHAKAMA KUU KUANZISHWA KATIKA MKOA WA MARA

Published in Jamii

Na Lydia Churi- Musoma

Mahakama ya Tanzania inakusudia kuanzisha Mahakama Kuu katika mkoa wa Mara ambapo ujenzi wa jengo la mahakama hiyo unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu.

Akizungumza leo mjini Musoma katika ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za kimahakama katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman alisema mkoa wa Mara unayo haki ya kuwa na Mahakama Kuu kwa kuwa nia ya Mahakama ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Alisema mahakama hiyo itajengwa kwa haraka na itamalizika katika kipindi cha mwaka moja kwa kuwa fedha kwa ajili ya ujenzi huo tayari imeshatengwa ambapo nyingine imetokana na msaada waliopewa kutoka Benki ya Dunia.

Alisema kuanzishwa kwa mahakama hiyo katika Mkoa wa Mara kutawapa fursa wananchi wa Mara ya kupata huduma kwa karibu zaidi na pia itasaidia kupunguza kesi zilizoko mahakamani kwa haraka.

Awali akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake alipomtembelea, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo alimwomba Jaji Mkuu kuanzisha Mahakama Kuu katika mkoa wake kwa kuwa asilimia 55 ya kesi zote za mauaji katika Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinatoka katika mkoa wa Mara hivyo mkoa huo unayo haki ya kuwa na Mahakama Kuu.

Pamoja na mkoa huo kuwa na kesi nyingi za mauaji, Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa wa Mara pia unakabiliwa na kesi nyingi zinazohusu masuala ya ardhi kwa kuwa ni asilimia 38.3 tu ya eneo zima la mkoa huo ndiyo eneo linalotuwa kwa ajili ya makazi ya watu na shughuli za maendeleo

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Mkoa wa Mara una wakazi zaidi ya milioni 1.3.

Alisema Mkoa wa Mara una eneo lenye kilometa za mraba 30,150 ambapo asilimia 36 ya eneo hilo ni maji wakati asilimia 25.7 ni eneo lenye mapori na hifadhi za Taifa ikiwemo mbugaya wanyama ya Serengeti.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa aliisifu Mahakama ya Tanzania kwa kufanya kazi yake kwa weledi ya kuzimaliza kesi zilizohusu mapigano ya koo zilizokuwepo katika siku za nyuma mkoani humo kwa kuwa zimesaidia maeneo ya mkoa huo kuwa salama hivi sasa na hayaonyeshi dalili za kujirudia. Aliongeza kuwa eneo la haki likitulia hata masuala ya utawala yakuwa rahisi.

Jaji mkuu Leo amehitimisaha ziara yake katika kanda ya Mwanza yenye mikoa ya Mara, Geita na Mwanza ambapo alikuwa akikagua shughuli mbalimbali za kimahakama katika kanda hiyo.(P.T)

Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo

Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam.

Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.

Picha ya pamoja. (P.T)

Wafanyakazi wataka Waziri aondolewe

Published in Jamii

Waziri Fabiano Silveira anayetuhumiwa kwa Rushwa

Wafanyakazi katika wizara inayopambana na rushwa nchini Brazil wameshindikiza kuondolewa kwa waziri wake mpya.

Maandamano hayo yanafuatiwa kutolewa kwa video ambayo Fabiano Silveira anatuhumiwa kusikika akikosoa uchunguzi wa rushwa katika kampuni ya mafuta ya serikali,Petrobras.Juma lililopita waziri wa mipango wa nchi hiyo alilazimishwa kuachia madaraka baada ya kukumbwa na shutuma kama hizo.Viongozi wote hao wawili walichaguliwa baada ya Rais Dilma Rousseff alipoondolewa madarakani.Amekuwa akisisitiza kwa muda mrefu kuwa mashitaka yaliyoundwa dhidi yake ni kwa ajili tu ya kuzuia upelelezi.BBC

1

Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.

Martin alisema, “Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu” 

 “Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira” aliongezea Martin.

Aidha, Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya na Amerika.

Mmari aliongezea, “Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali, usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa kwenye programu”

2

Wanafunzi wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.

Kwa upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo  wameshukuru kwa nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.

Mmoja wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha,  alisema kuwa anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia kutatua matatizo hayo.

“Nimekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania” aliongezea Bi. Malamsha.

3

Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao

Naye kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha biashara.

“Nimeweza kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe” alimalizia Said.

Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo  la kuisaidia jamii ya Tanzania sehemu mbalimbali.(P.T)

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

Magazeti ya Leo Jumanne

Published in Jamii

Ndugu zangu,

Mengine yanayotokea kwenye jamii yetu unabaki kushangaa. Na Magufuli huyu amekuja na tiba-mshtuko yenye kufaa.

Na unapomsoma Mwandishi Naomi Klein kuna ya kuyatafakari kuhusu nchi yetu na hususan juu ya uongozi wetu na hatma ya taifa letu.

Ni kama alivyobainisha Mwalimu Nyerere kupitia kitabu chake chenye jina hilo.

Hakika, naziona fikra za Nyerere pia kwenye maandiko ya Naomi Klein. Nami nafikiria pia falsafa ya uongozi wetu na vichwa vya samaki.

Ndugu zangu,

Kama kichwa cha samaki kinatoa harufu ya uozo, basi, ni uwendawazimu kudhani kuwa dawa ni kukata kichwa cha samaki.

Kimsingi, samaki mzima atakuwa ameoza. Ni sawa pia na jibini kwa maana ya cream ya maziwa. Kama jibini haina ubora, basi, tatizo ni ubora wa maziwa. Maana jibini inatokana na maziwa. Jamii ndio maziwa. Je, kama hatujengi jamii iliyo bora kwanini tudhani tutapata ' viongozi-jibini' walio bora?

Tuukubali ukweli, kuwa kama nchi tuna tatizo kubwa kwa viongozi na watendaji wetu wengi, si wote, kuwa ni matokeo ya jamii- maziwa isiyo bora. Tufanye nini? Jadili...
Ni Neno la Usiku.
Maggid,
Iringa.(P.T)

- Nilipoishi Maisha Ya Kijijini, Igagala 1991..!

Ndugu zangu,

Pichani nikichota maji ya kisima kijijini Igagala, kilomita 16 kutoka Njombe Mjini. Ni Juni mwaka 1991. Ni baada ya kumaliza kulitumikia taifa kwa mujibu wa sheria, JKT, Operesheni Kambarage, 90-91.

Kwa mwaka mmoja nilifanya kazi za kujitolea kwenye Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Ulembwe. Hapo nilipewa nyumba ndogo ya kuishi na shamba la ekari moja. Kijijini hakukuwa na umeme wala maji ya bomba. Na wala hakukuwa na mawasiliano ya simu. Nilisikiliza sana redio, na zaidi BBC Focus of Africa, na BBC Network Africa.

Nakumbuka wanakijiji Igagala walikuwa watu wema sana. Nilijifunza mambo mengi kutoka kwao, nao kuna waliojifunza kutoka kwangu.

Kuna waliyoshangaa kijana msomi kuamua kuishi kijijini na kufanya kazi ya kujitolea, ikiwamo kilimo pia. Na kuna waliodhani nimetumwa kazi maalum ya kitafiti.

Maisha ya kijijini yaliifanya imani yangu katika Ujamaa na Kujitegemea kuongezeka mara dufu.

Bado naamini, kuwa hali zile za maisha ya watu wa vijijini kamwe haziwezi kuwa za nafuu kwenye mfumo wa kibepari.
Maggid,
Iringa.(P.T)

Uamuzi wa kesi ya Hissenne Habre kutolewa

Published in Jamii

Hissene Habre

Mahakama mmoja nchini Senegal inatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya kiongozi wa zamani wa Chad Hissenne Habre.

Ni kesi ya kwanza ulimwenguni , kwa mahakama ya nchi kumshtaki kiongozi huyo wa zamani kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu.

Mwendesha mashtaka katika mahakama maalum ya Afrika, ambayo iliundwa na Umoja wa Afrika mjini Dakar ametoa ombi la kumtaka Habre kufungwa kifungo cha maisha.

Bwana Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati wa utawala wake miaka ya 80, madai ambayo ameyakana

Habre alikamatwa nchini Senegal , na kupelekwa uhamishoni mwaka 2013.BBC

MAREHEMU JACKLINE OSWALD KAPINGA

Familia ya Marehemu Mzee Oswald Kapinga ya Sinza – Dar e salaam (karibu na white inn) inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Jacqueline kilichotokea jana tarehe 29/05/2016 katika hospitali ya muhimbili jijini Dar es salaam.

Familia inapenda kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ya kuwa, msiba utakuwa nyumbani kwa wazazi wake hapo sinza.

Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika, taarifa ya awali kutoka kwa familia, Marehemu wanategemea kumuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele siku ya kesho (Jumanne) ya Tarehe 31/05/2016 katika makaburi ya sinza karibu na Ukumbi wa mwika kuanzia saa 8.00 Mchana.

Kwa taarifa zaidi na maelekezo mbali mbali unaweza kuwasiliana na makaka wa marehemu hapo chini:

JOSEPH O. KAPINGA (Mwananchi communication) – 0788617654

GOSBERT O. KAPINGA – 0754286301

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA,

JINA LAKE LIHIMIDIWE

AMEN.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma.

 Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa Bunge leo mjini Dodoma.(P.T)

Read more...

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

mjengwaapp_copy_4d310.jpg

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Wanakijiji

BLOG SHABIHANA